Mwanzo. Chapter 10
1 Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika.
2 Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi.
3 Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.
4 Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani.
5 Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao.
6 Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.
7 Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani.
8 Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
9 Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za Bwana.
10 Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.
11 Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala;
12 na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa.
13 Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi,
14 na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori.
15 Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi,
16 na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi,
17 na Mhivi, na Mwarki, na Msini,
18 na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Baadaye jamaa za Wakanaani walitawanyikana.
19 Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha.
20 Hao ndio wana wa Hamu, kufuata jamaa zao, kwa lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao.
21 Naye Shemu ambaye ni baba wa wana wote wa Eberi, na ndugu mkubwa wa Yafethi, akazaliwa wana.
22 Wana wa Shemu ni Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu.
23 Na wana wa Aramu ni Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi.
24 Arfaksadi akamzaa Sela, Sela akamzaa Eberi.
25 Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza ni Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye ni Yoktani.
26 Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera,
27 na Hadoramu, na Uzali, na Dikla,
28 na Obali, na Abimaeli, na Seba,
29 na Ofiri, na Havila, na Yobabi. Hao wote ndio wana wa Yoktani.
30 Makao yao yalikuwa kutoka Mesha kwa njia ya Sefari, mlima wa mashariki.
31 Hao ndio wana wa Shemu, kufuata jamaa zao, na lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao.
32 Hizo ndizo jamaa za wana wa Nuhu, kufuata vizazi vyao, katika mataifa yao; na kwa hao mataifa yaligawanyika katika nchi baada ya gharika.